kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel na mkurugenzi wa kampuni ya Binslum Tyre wakionesha flana zenye nembo ya kampuni ya Binslum Tyre Katibu wa Timu ya Mbeya city, Emmanuel Kimbe, akiishukuru kampuni hiyo kwa udhamini wa timu yao ya Mbeya city Na kevin sambo jr TIMU ya Mpira wa miguu ya Mbeya City Fc inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeanza kujihakikishia kufanya vizuri zaidi kwa msimu ujao baada ya kupata rasmi mdhamini. Kampuni ya Bin Slum Company Limited yenye makao makuu jijini Dar Es Salaam ndiye kampuni ya kwanza kukubali kuwa mdhamini wa timu hiyo kwa miaka miwili kwa kitita cha shilingi Milioni 360. Utilianaji sahihi wa mkataba umefanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mbeya baina ya Uongozi wa Kampuni hiyo na Halmashauri ya Jiji la Mbeya mbele ya vyombo mbali mbali vya habari. Akizungumza na vyombo vya habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Binslum, alisema ...